TISHETI YA KIKWETE YAWA GUMZO


20210525_221947.jpg

 KWA kawaida Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ni mtu mwenye tabasamu muda mwingi usoni kwake. Ni nadra kumuona akiwa amefura kwa hasira.

Maandishi yaliyoandikwa katika tisheti anayoonekana ameivaa, ni kama yamewachanganya watu, kwani hayaendani na uhalisia wake. Imeandikwa hivi: KASI ISAMBAZAYO TABASAMU.

Sawa, yeye ni shabiki wa Yanga, lakini mabingwa hao wa kihistoria wana kasi gani inayosambaza tabasamu kwa mashabiki wake?

Bila shaka hiki ni kijembe cha kisiasa kwa wanasiasa.

Maneno haya yana maana kubwa sana yanapokaa mgongoni mwake tofauti na yangekaa mgongoni mwa mwananchi wa kawaida.


No comments