DIAMOND AIWAKILISHA TZ TUZO ZA BET 2021

TUZO kubwa za BET zinazojumuisha mastaa mbalimbali wa muziki duniani, zimetoa orodha ya watakaowania hadhi hiyo kwa mwaka 2021 na kwa namna ya kufurahisha, msanii Diamond Platnum ametajwa kuwemo mashindanoni.
Katika kipengele cha Best
International Act, kijana huyo kutoka kitongoji masikini cha Tandale jijini Dar
es Salaam, ametajwa kuiwania tuzo hiyo akishindana na wakali wengine ambao ni Wizkid
na Burna Boy wa Nigeria, Emicida wa Brazil, Headie wa UK, Aya Nakamura wa
Ufaransa, Youssoupha wa Ufaransa na Young T & Bugsey wa UK.
Tuzo zinatolewa June 28, 2021

Post a Comment