RAIS AKUTANA NA TAJIRI NAMBA MOJA AFRIKA


D1.jpg

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani, leo amekutana na kufanya mazungumzo na tajiri namba moja barani Afrika, Alhaji Aliko Dangote, Ikulu jijini Dar es Salaam.


Alhaji Dangote ambaye ni Mnigeria na mfanyabiashara mkubwa duniani, ni mwekezaji nchini Tanzania akiwa amewekeza katika Kiwanda Cha Saruji cha Dangote kilichoko mkoani Mtwara.

Alhaji Dangote amemshukuru Rais Samia kwa kuboresha mazingira ya Uwekezaji nchini na ameahidi kuwa ataendelea kuwekeza Tanzania kwenye maeneo tofauti ikiwamo ujenzi wa Kiwanda cha Mbolea,

Kwa upande wake, Rais Samia aliahidi kuwa Serikali yake itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini kwa faida ya pande zote na aliwaagiza mawaziri husika kushughulikia changamoto zinazoikabili Kampuni ya Dangote.

 

No comments