ASIMULIA ALIVYOKUTANA NA USHIRIKINA SITE


Tips for buying used excavators


JAMAA mmoja Mtanzania, ambaye alilelewa katika mazingira ya dini tangu utoto wake, anasimulia jinsi alivyoacha kazi na kuamua kujiingiza katika kujiajiri kwenye machimbo na vitu alivyokutana navyo.

Simulizi hii ni credit kwa Jamii Forum:

"Kwanza nitajikita kwenye mada kutokana na personal experience ya hapa home Tz. Binafsi nimekulia mazingira ya dini sana, kwa hiyo mambo ya uchawi au ku-practice masuala ya kiganga /jadi sikuwahi.

"Lakini kwa uzoefu na namna nilivyoona katika kutembea mikoa ya hapa Tanzania, hasa huko vijijini watu wamelazimika kutofanya Maendeleo, kuyahama makazi yao kwa kuogopa kulogwa. Unakuta eti Kijijini mtu alikuwa hawezi kujenga nyumba nzuri na kuezeka bati, ukifanya hiyo kitu unaanza kuandamwa na mambo mengine kama hayo.

Personal Experience.

"Nilipoamua ku-resign kazi na kuanza mishe zangu binafsi, niliingia kwenye kazi za mining na huku ndio nilikutana na hayo mambo.

"Tulienda kuanzisha mining site Handeni- Tanga. Aisee, nilikuwa nausikia tu ushirikina sasa kule ndio nilienda kuona. Yaani mtu analoga machine (Excavator) inakuwa haifanyi chochote, tunaita mafundi wa kila aina wanachokonoa wee ila waapi, na machine bado mpya.

"Baadae one of the labors niliokuwa nao pale site akaniita na wenzake pembeni, wakaniambia ndugu yetu, hapa kutakuwa na kitu kimefanyika, wakanitaka twende na mganga ili tuka unlock. Mimi nikawa siamini kama mashine inaweza logwa na sikuwa na imani na zile mambo kabisa.

Basi nikawauliza kama wanaweza kwenda wenyewe wafanye kwa niaba, wakasema poa niwape elfu 20 wanunue kuku, basi mshikaji akanambia tuwape. Mini nikawapa wakaondoka bwana, hapo tumehangaika na fundi wiring na hydrologic system wote wanasema hawaona tatizo, ila machine haina kabisa nguvu ya kuchimba.

"Wale wadau walirudi time za jioni kama saa kumi na moja hivi, na maji yenye dawa kwenye chupa pamoja na vimiti viwili. Wakasema Operator wa machine aweke mfukoni kimti kimoja na kingine aweke chini ya seat yake, na yale maji ya dawa imwagiwe machine na kuzunguka eneo la mgodi. Operator akasema fresh ,yeye alikuwa anaamini sana, wale jamaa wakamwaga maji kwenye machine nakuzunguka pale site, na mwingine akaenda akaleta ka kuku kadogo akachimba shimbo pembezoni mwa site akakafukia kale kakuku kakiwa kazima.

"Baada ya hapo wakamwambia Operator awashe machine . Mi naangalia tuu kama movie, aisee huwezi amini, machine ikawa na power kuzidi hata uwezo wake siku zote. Nikashangaa sana, jamaa wale wenyeji wanacheka wananiambia "karibu Tanga mgosi".

"Hii ni kwa ufupi tuu, nina mengi sana nime experience sehemu mbali mbali hasa katika kazi ya mining, maana mnaenda kuanzisha kazi sehem porini kumbe palikua ni mahali pa matambiko, basi vituko ni vingi nikijaaliwa muda nitakuja andika matukio mengine . Watu wana uwezo wa kupoteza madini aridhini, yaani unachimba wee na kuunguza hela ila huoni kitu, wakati mwanzo mambo yalikua fresh kabisa. Lakini mwisho wa siku nina Imani na Mungu , hatutakiwi kuweka Imani kwa waganga kwa sababu nao ni binadamu, uchawi upo na Mungu yupo.

"Serikali haiamini katika uchawi, ni sawa kabisa lakini ukweli ni kwamba uchawi umelostisha sana watu, pengine watu wangekuwa na maendeleo sehemu mbali mbali isingekuwa haya mambo. Siku hizi kidogo yanapungua ,nadhani muingiliano wa wageni na wenyeji sehemu mbalimbali unafanya watu ku-focus kwenye maendeleo. I'm not sure kama tumeshawahi kuwa na sheria inayokemea haya mambo kwa kuwa ni invisible world."

Naomba niishie hapo kwa leo, najua wengi wetu tuna experience tofauti tofauti, kuwa huru ku share nasi tujifunze kitu.

No comments