FRED VUNJA BEI APENYA UVCCM

YULE mfanyabiashara wa nguo aliyeshinda dili kubwa la zaidi ya bilioni mbili ili kuuza na kusambaza jezi za Simba, amepenya tena, safari hii ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).
Mfanyabishara huyo
mwenyeji wa Makete mkoani Iringa, Fredy Ngajiro Maarufu Kama Fred Vunjabei
ameteuliwa Kuwa Mwenyekiti Wa Kamati Ya Fedha Ya Uvccm.
Fred Ngajiro amepitishwa
na Baraza kuu la UVCCM kuwa Mwenyekiti mpya wa kamati ya Uchumi, Uwezeshaji na
Fedha kupitia kikao cha Baraza Kuu ambacho kimemalizika jana Makao Makuu ya CCM
Dodoma.
Kamati ya
utekelezaji chini ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James ilikuja na
pendekezo la jina la mwenyekiti huyo wa kamati ambapo baadae alithibitishwa na
wajumbe kwa kura nyingi za ndio huku katibu wake akifahamika kwa jina la Rose
Manumba, Baraza lilichagua wajumbe wengine wanne wa kamati kutoka bara na
visiwani.

Post a Comment