PUMZISHA AKILI KIDOGO MPENDWA

PROFESA alipoingia darasani alianza
na mada nzito sana.
Wakati alipogeukia ubaoni, mmoja wa wanafunzi alipiga filimbi.
Aligeuka, akatazama darasa na akauliza jina la aliyepiga
filimbi.
Hakuna aliyejibu.
Profesa kwa amani aliweka kalamu mfukoni akasema:
"Tuachane na hilo Mada inaishia hapa nitawasimulia
hadithi ili tumalizie muda uliobaki ".
Kila mtu alivutiwa.
"Jana usiku nilijitahidi kulala, lakini usingizi ulikuwa
mbali na macho yangu, kwa hivyo nilifikiri bora nijaze petroli kwenye gari
langu, nisipoteze wakati wangu kitandani alafu asubuhi ndio nipate usingizi.
Baada ya kujaza mafuta kwenye tanki langu, nilianza kuzurura
katika eneo hilo, huku nikifurahiya amani ya kusafiri bila kusumbuliwa na
trafiki.
Ghafla, kwenye kona nikamwona msichana mdogo mrembo ni mdogo
sawa na nguo alizokuwa amevaa.
Lazima alikuwa anarudi kutoka disco au sherehe.
kwa heshima, niligeuza gari langu kuelekea kwake na kumuuliza
ikiwa ninaweza kumpa msaada wowote.
Aliniomba akasema atafurahi kama ntamuacha nyumbani kwao,
nilikubali.
Alikaa kwenye kiti cha mbele na mimi.
Tulianza kuongea, na nilimshangaa alikuwa mwerevu sana,
alikuwa anajua kujenga hoja na mada nyingi ambazo vijana wengi hawana.
Tulipofika nyumbani kwao, alikiri kwamba nina tabia njema na
naheshimu wanawake alikili kwamba ananipenda.
Nilimkubalia kutokana na akili na uzuri wake hatamimi
nimeanza kumpenda.
Nilimwambia juu ya kazi yangu kama profesa katika chuo kikuu.
Msichana aliniomba namba yangu, ambayo nilimpa kwa hiari.
kisha akaniomba jambo moja, ambalo ni singeweza kukataa
kawaida.
Alisema kuwa kaka yake ni mwanafunzi katika chuo kikuu hapa,
na akaniombaa nimtunze vizuri, kwani tutakuwa na uhusiano wa kudumu.
Nikamuomba jina la huyo mwanafunzi.
Alisema kuwa nitamtambua kwa ubora wake mashuhuri sana,
Ni mpiga filimbi anapiga vizuri sana!
Macho yote darasani yakamgeukia yule kijana aliyepiga filimbi.
Profesa akasema:
"Aisee Sikununua Ph.D yangu kwa wana Saikolojia ..
Nimepata kwa kusoma. ” Oya! Toka nje wewe

Post a Comment