OLE SABAYA AKAMATWA, ANAHOJIWA

ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ambaye alisimamishwa na Rais Samia Suluhu Hassan ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili, imeripotiwa kuwa kiongozi huyo amekamatwa na vyombo vya dola na sasa anahojiwa.
Kwa mujibu wa
vyanzo vya uhakika, Sabaya amehojiwa na vyombo vyote vya dola na wakati wowote
atapandishwa kizimbani.
Miongoni mwa tuhuma
dhidi yake ni pamoja na kuwabambikia watu kesi, kuhusika kupora fedha kwa
kutumia nafasi yake, kunyanyasa raia na kufanya kazi zisizomuhusu, kama kudai
kodi.

Post a Comment