NANI KAMUUDHI PROFESA JAY?


Professor Jay loses seat in Tanzanian elections – Nairobi News

 UTANIAMBIA NINI ndiyo ngoma mpya ya mkongwe wa Hip Hop Tanzania, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay iliyotoka wiki chache zilizopita na sasa inapata mileage ya kutosha katika redio nyingi hapa nchini.

Ukisikiliza mashairi ya mkongwe huyo, unaona kabisa kaimba kwa hisia, kitu kama kimemuuma kwa muda mrefu na sasa kaamua aseme.

Tena aliyemkera anaonekana kuwa bwa mdogo tu, maana ndani ya wimbo huo anasema 'Utaniambia nini, nimeanza kuimba kabla yako. Nimeshakula sana bata kabla yako na kama ni ng'ambo, nishatimba kitambo kabla yako.

'Hata mjengoni nilikuwa na baba yako au mama yako..... yaani kifupi, Mzee wa Mitulinga kachafukwa.

Nani kamkera, Ojuku Blog inamtafuta amwage ukweli...

No comments