DIAMOND, HARMONIZE WAWEKWA TIMU MOJA NA WAZIRI


AGIZO LA WAZIRI WA TAMISEMI MH:SELEMANI JAFO KWA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI  NCHINI.

 WAKATI ikifahamika kuwa wasanii wawili wakubwa, Diamond Platnum na Konde Boya, Harmonize hawaivi chungu kimoja, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo amewateua wawili hao kuungana kuwa mabalozi wa Uhamasishaji Utunzaji wa Mazingira Nchini.

Pamoja nao, pia Waziri Jafo amewatangaza watangazaji Masoud Kipanya na Milardi Ayo kuwemo katika timu hiyo akisema amewateua kutokana na ushawishi wao kwa Jamii ili kuhamasisha utunzaji wa mazingira na upandaji miti.
Mabalozi wengine walioteuliwa ni pamoja na Haji Manara, Antonio Nugaz, Nandy, Idris Sultan, Monalisa, Mbunge Esther Matiko, Mbunge Joseph Musukuma na Mwandishi wa Radio Uhuru Sakina Abdulmasoud na May Zumo.

 

No comments