KOCHA ATUKANWA KWA KUITOA TIMU YAKE YA ZAMANI


Inaweza kuwa picha ya mtu mmoja au zaidi

MASHABIKI wenye hasira wa timu ya Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini, walimshambulia kwa matusi na maandamano kocha wa klabu ya Al Ahly, Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini baada ya kuitupa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kabla ya kuifundisha Al Ahyl, Mosimane alikuwa ni kocha wa mabingwa hao wa Afrika Kusini.

Mashabiki walivamia basi walilopanda wachezaji wa Al Ahly kwa maandamano huku wakiwa wamebeba mabango yalioandika jina la kocha Pitso na yenye matusi.

Al Ahly iliifunga Mamelod mabao 2-0 katika mchezo wa robo fainali ya kwanza uliopigwa nchini Misri na mchezo wa robo fainali ya pili uliochezwa Afrika Kusini ulimalizika kwa sare ya 1-1 hivyo Mamelod wanatupwa nje kwa jumla ya mabao 3-1.

Kitendo hicho kiliwachukiza sana baadhi ya mashabiki wa klabu ya Mamelod na kuamua kumshambulia kocha Pitso.

 

No comments