MORRISON ATHIBITISHA THAMANI YAKE NDANI YA SIMBA


VIDEO: Morrison on song as Simba win Tanzania Community Shield |  Footy-GHANA.com

 IKICHEZA mechi yake ya 26 leo katika Uwanja wa Majaliwa kule Luhangwa, Lindi, timu ya Simba ilikuwa nyuma kwa bao moja hadi wakati wa mapumziko.

Wengi wakiamini kwamba huu utakuwa mchezo mgumu kwa mabingwa hao watetezi, na hasa baada ya Namungo kuanza kujiangusha ovyo wakiamini wanashinda, kocha Didier Gomes Da Rosa alifanya mabadiliko kwa kuwatoa Larry Bwalya, Meddie Kagere na Konde Boy, wakitoa nafasi kwa Hassan Dilunga, John Bocco na Benard Morrison.

Wakiwa nyuma kwa bao hilo moja, Simba walisawazisha kupitia kwa Chris Mugalu, aliyeungankisha krosi kutoka kwa beki Shomari Kapombe ambaye alipenyezewa penetration pass na HD.

Simba wakapata bao la pili ambalo lilifungwa na John Bocco kufuatiwa pasi safi kutoka kwa Mugalu, ambaye naye alipewa pasi ile na HD.

Lakini burudani ya wanamsimbazi ilihitimishwa na Bernad Morisson ambaye alithibitisha thamani yake ndani ya kikosi hicho.

Hassan Dilunga alilazimika kulala ili kuutoa mpira miguuni mwa mchezaji wa Namungo katikati ya uwanja, mpira huo ukamfikia Morisson, ambaye aliusogeza kidogo tu kutoka umbali wa zaidi ya mita 40, akamtazama kipa wa Namungo kisha akaupiga mpira mrefu uliomaliza mechi ya leo kwa Simba kushinda kwa bao 3-1.

No comments