MO: SITANUNUA FERARI TENA NA ROLLS ROYCE, NITAWEKEZA ZAIDI SIMBA

MWEKEZAJI
wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Mohamed Ghulam Dewji maarufu kama
Mo, amesema amesitisha mpango wake wa kujizawadia gari la kifahari aina ya
Ferari aliokua amepanga na badala yake atawekeza zaidi kwa timu yake ili kuwapa
furaha watu wengi zaidi.
Kupitia
katika akaunti yake ya Instagram, tajiri huyo namba moja kijana barani Afrika
amesema furaha ya mashabiki wa Simba kwake ni muhimu zaidi kuliko furaha yake
binafsi.
Maelezo
hayo, bila shaka, yanakuja baada ya jana kuishuhudia timu yake ikipokea kipigo
cha mbwa mwizi cha mabao 4-0 kutoka kwa Kaizer Chiefs katika mchezo wa kwanza
wa robo fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kule Johannesburg Afrika
Kusini licha ya timu yake kutandaza soka safi.

Post a Comment