MO AKANDIA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA


Mapinduzi Cup: Simba SC chairman Dewji resigns after losing the final |  Goal.com

 KATIKA kile kinachotafsiriwa kama hasira, mwekezaji ndani ya Simba, Mohamed Ghulam Dewji maarufu kama Mo, amesema nusu fainali ya Ligi ya Mabigwa Afrika, haitakuwa na mvuto pasipo uwepo wa timu yake ya Simba.

Hii inakuja baada ya wekundu wa Msimbazi, wakicheza soka safi katika mechi zote mbili za robo fainali dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kutolewa kwa jumla ya mabao 4-3.

Katika mchezo wa kwanza jijini Johannesburg Afrika Kusini, Simba ilipokea kipigo 'hevi' cha mabao 4-0 na kwenye marudiano Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, wekundu hao wa Msimbazi wakawapiga Kaizer mabao 3-0.

 

No comments