MKOA WA CHATO WAZIDI KUPINGWA


Prof Anna Tibaijuka to refund Sh1.6billion Tegeta-Escrow money - The Citizen

 HUKU michakato ikiwa imeanza kwa ajili ya kuiwezesha Chato kuwa Mkoa, wadau mbalimbali wamepinga jambo hilo na kudai watu waache kumshinikiza Rais Samia Suluhu Hassan kukubali kitu hicho, bali ashauri kwa nia ya kujenga.

Aliyewahi kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alisema hakubaliana na suala hilo, kwa vile anaamini eneo hilo jirani na nyumbani kwao, halina sifa za kuwa mkoa.

Pamoja na kuorodhesha sababu nyingi za kutokidhi vigezo, lakini kubwa alilosema ni nchi kuacha kutoa maamuzi yenye lengo la kuwaridhisha wakubwa, badala yake ifikirie mzigo mkubwa unaokwenda kwa walipa kodi.

Mwingine aliyepinga jambo la Chato kuwa mkoa, ni Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge-Ngara Mhashamu Baba Askofu Severine Niwemugizi  ambaye alitumia Dominika ya leo kutoa hisia, maoni zake kuhusu kuifanya Chato kuwa Mkoa.

Mwingine aliyepinga wazo hilo ni Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.

 

No comments