MJUE RAIS MASIKINI KULIKO WOTE DUNIANI

 

JOSE Alberto Pepe Mujica Cardano, ni Rais wa 40 wa nchi ya Uruguay, akitawala kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, mzaliwa wa Montevideo mwaka 1935. 

Umasikini wake ulitokana na kitendo chake cha kuchangia zaidi ya asilimia 90 ya mshahara wake wa dola za kimarekani 12,000 katika shughuli mbalimbali za kijamii na hasa kwa watu wenye uhitaji.

Mara baada ya kuchaguliwa, alikataa kwenda kuishi Ikulu na badala yake akasalia nyumbani kwake

akitumia usafiri wa gari aina ya Volkswagen bittle kipindi chote alichokuwa madarakani.

Katika hali ya kushangaza, alipoenda kupata matibabu hospitalini, alipanga foleni kama wagonjwa wengine.

Kipindi cha machafuko ya Syria alichukua watoto 100 na kuwalea na maisha ya nyumbani kwake yalikuwa ya kawaida sana, huku mwenyewe akishiriki kikamilifu shughuli za kilimo.

 

 

No comments