MIAMBA WATATU DAR WAINGIA NUSU FAINALI FA


Dailynews

 SIMBA, Yanga na Azam, miamba ya soka Tanzania Bara ambao wanafukuzana kuwania ubingwa wa soka msimu huu, wote wamefanikiwa kuingia nusu fainali ya Michuano ya Azam Confederation Cup maarufu kama FA Cup msimu huu.

Hiyo inafuatia ushindi wao katika mechi za robo fainali, Yanga ikiiondoa Mwandui FC katika mchezo wao wa robo fainali, Azam wakiibenjua Rhino Rangers ya Tabora wakati Mabingwa wa nchi, wakipata ushindi mbele ya Dodoma Jiji.

Katika nusu fainali, mabingwa wa kihistoria Yanga, watapepetuana na Biashara Mara wakati vigogo wawili wa Dar es Salaam, Simba na Azam, wakimtafuta wa kufika fainali.

Simba ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo.

No comments