MAMA AMTUHUMU MWANAE KUIBA BUKU TANO, AJINYONGA

MAMA mmoja aitwaye Ashura Selemani anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Kibaha baada ya mwanaye mwenye umri wa miaka 14 kujiua kwa kujinyonga kufuatia kumtuhumu kuwa alimuibia kiasi cha shilingi elfu tano.
Mtoto huyo wa kike alikuwa ni mwanafunzi
wa darasa la saba Shule ya Msingi Mtongani.
Akizungumza leo Jumatano Mei 26, 2021 Kamanda wa Polisi
mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa amesema tukio hilo limetokea juzi Jumatatu Mei 24,
2021 na uchunguzi ulipofanyika ilibainika chanzo cha kifo kutuhumiwa kuiba
kiasi hicho cha fedha.
"Ni kweli tukio hili limetokea, lakini sisi Jeshi la polisi
tulipofanya uchunguzi wetu tukabaini huyu mtoto aliamua kujitoa roho kwa sababu
mama yake mzazi, Ashura Selemani alimtuhumu kumuibia pesa ambayo ilikuwa ya
mama huyo.”
“Tunamshikilia mama huyo pamoja na baba mlezi (jina
linahifadhiwa) kwa mahojiano zaidi,” amesema.
Credit: Mwananchi

Post a Comment