MATEJA NI HATARI KIGAMBONI- MKUU WA WILAYA

MKUU wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafri amethibitisha kuwa eneo lake linaathiriwa vibaya na madawa ya kulevya, kwani makumi ya watu wanaletwa katika vituo vya kutoa huduma za kuwasaidia waathirika kila mwezi.
“Sasa hivi Wilaya ya Kigamboni kila mwezi tunapata waathirika
50 wa dawa za kulevya wanaofika kwenye kituo chetu cha Vijibweni ambao kwa
mwaka ni Waathirika 600 kwenye kituo hiki, ni wengi sana ukilinganisha na vituo
vingine,” amesema DC Sarah Msafiri.
“Pia tumetembelea na sober house zetu, tumetembelea Pili
Misana Sober House ambao kwa miaka 8 wamehudumia waathirika sio chini ya elfu
moja, tumekwenda kituo kingine cha The Waited Rehab na kina kama mwaka mmoja na
tayari amepokea Wagonjwa 32, unaweza kuona athari zilivyo kubwa,

Post a Comment