MANENO YA KOCHA WA YANGA PRINCESS, EDNA LEMA

 Full-time Yanga Princess 4:0 Tanzanite... - Yanga Fans Family | Facebook

 

Alhamdulilah..
Tumemaliza ligi salama, tunashukuru kwa nafasi tuliyomaliza point moja nyuma ya aliyetwaa ubingwa, naweza kusema lengo moja la kuijenga timu sisi kama benchi la ufundi tumefanikiwa ukiangalia tulipoitoa timu, tumeifanya Yanga Princess kuwa timu bora na yenye ushindani msimu huu.

Mafanikio ni hatua, naamini hapa ilipofika timu ndio sehemu sahihi ya Uongozi kuijenga timu na kuwa bora zaid ya hapa kuelekea kwenye mafanikio, niwapongeze wachezaji wangu pamoja na benchi zima la ufundi likiongozwa na mimi tulifanya kila tulichoweza lakini haukuwa wakati wetu.

Hatupaswi kusononeka tunapaswa kushukuru kwa kila jambo na kuamini kila jambo hutokea kwa sababu na kilichochotekea leo ndicho Mungu alikuwa amekipanga naaamini wakati wetu upo na utafika. Naamini kilichotokea msimu huu kitaamsha ari mpya ya kutamani mafanikio makubwa.

Nawashukuru washabiki wote wa Yanga kwa kipindi chote cha ligi kwa sapoti yenu, msiumie wala msikate tamaa endeleeni kusapoti timu zenu zote wakati wote, hakuna nyakati za kudumu itafika wakati furaha yenu itarejea kwa uwezo wa Allah. Wakati sahihi ni wakati wa Mungu.

Daima mbele...Nyuma mwiko💚💚💛💛

No comments