MAKAMU WA RAIS MALI ACHUKUA MADARAKA

MAKAMU wa Rais wa Mpito Nchini Mali, Kanali Assimi Goita amechukua
madaraka baada ya Rais wa Mpito na Waziri Mkuu kushindwa kumshirikisha katika
uundaji wa Serikali.
Goita ambaye aliongoza Mapinduzi ya Kijeshi yaliyotokea
Agosti 2020, amesema alielekeza kushikiliwa kwa viongozi hao baada ya wenzake
wawili walioshiriki Mapinduzi kuondolewa kwenye nafasi zao Serikalini.
Amewahakikisha wananchi kuwa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika
mwaka 2022 ili kupata viongozi waliochaguliwa utaendelea kama ilivyopangwa.

Post a Comment