HOROYA YAMTAKA MUKOKO KWA MILIONI 460

MIAMBA wa soka Barani Afrika, Klabu
ya Horoya inataka kumnunua kiungo mkabaji wa Yanga, Mukoko Tonombe huku
wakiweka ofa kubwa ya mshahara mara tatu ya ule anaolipwa Yanga.
Horoya inafahamu kwamba mshahara wa Mukoko ni dola 3100 (Sh 6milioni) pale Yanga kwa sasa na wamemwambia watamlipa dola 9000 (sh 18milioni) kwa mwezi.
Kwa mujibu wa mtandao wa Futbal Planet, licha ya mshahara huo, pia klabu hiyo itapeleka ofa ya awali kwa mabingwa hao wa kihistoria wa kiasi cha dola laki mbili, sawa na shilingi milioni 460 za Kitanzania ili kuwashawishi kumwachia kiungo huyo ambaye mkataba wake umebakiza mwaka mmoja kumalizika.
Kwa mujibu wa wakala wa mchezaji
huyo, Nestor Mutuale amethibitisha kuwa Horoya wanamtaka Mukoko na watatuma Ofa
rasmi mapema wiki hii.

Post a Comment