LAMINE MORO AMWAGA MBOGA UTOVU WA NIDHAMU
HUKU mashabiki wa soka nchini hususani wale wa mabingwa wa kihistoria Yanga, wakiamini kuwa nahodha na beki wao kisiki Lamine Moro ni mtovu wa nidhamu, mchezaji huyo leo amefunguka yote, kama alivyonukuliwa na Soka Letu:
"Wiki iliyopita kabla hatujasafiri kwenda Mtwara nilipata majeraja ambayo benchi la ufundi walikuwa wakifahamu, kwa hiyo tulipofika Mtwara, sikuweza kufanya mazoezi lakini nilikuwepo kwenye uwanja wa mazoezi pamoja na timu nzima.
"Kocha aliuliza madaktari kwa nini sifanyi mazoezi, akaambiwa kuhusu hali yangu kwamba nimepata majeraha. Kocha alisisitiza kwamba nilitakiwa kufanya mazoezi, nikamweleza kuhusu hali yangu kwamba sitaweza kufanya mazoezi.
"Tuliporudi hotelini akawaambia madaktari kwamba haamini kama kweli ninamajeraha, kwa hiyo wanatakiwa wanipeleke hispitali.
"Tulikwenda hospitali na walishuhudia kuwa nilikuwa nina majeraha, wakampelekea kocha ripoti ambayo aliiona yeye mwenyewe. Siku iliyofuata ilikuwa Ramadhani ya mwisho (mfungo wa mwisho kwa Waislamu) niliamka asubuhi nikiwa nimechoka kidogo na kuhisi msuli umekaza kwa hiyo sikwenda pamoja na wenzangu kwenye uwanja wa mazoezi.
"Baada ya mazoezi nilikutana na meneja wa timu akanieleza kwamba kocha anahitaji kikao cha pamoja na sisi, nikamwambia sawa nikaamua kufanya haraka kwenda kuswali kabla ya kikao kuanza.
"Niliporudi sikukuta mtu yeyote sehemu ambapo tulikubaliana kikao kingefanyika, nikarudi chumbani kwangu. Saa mbili baadaye, meneja wa timu akanipigia kunijulisha kwamba uongozi umesema natakiwa nirudi Dar es Salaam.
"Sikusema chochote
nikaondoka Mtwara lakini nilikutana na Engineer uwanja wa ndege wakati
naondoka.
Baadaye nikaona Bumbuli amepost Instagram kwamba sina nidhamu nilipigana na kocha na ameniamuru nirudi nyumbani [Dar].
"Nikampigia simu Engineer
na Dr. Msolla mara kadhaa lakini wote hawakupokea simu zangu.
Nilimtumia ujumbe Dr. Msolla
akasoma lakini hakunijibu chochote, nikaamua kukaa kimya. Hakuna aliyenipigia
tangu siku hiyo hadi Kaimu Katibu Mkuu aliponipigia leo [Mei 27] kwamba
wananihitaji ofisini."
- Amesema Lamine Moro
[@laminebenomar] Nahodha Yanga.

Post a Comment