DIAMOND AENDA MSABAHI SHAKA LUMUMBA


Habarileo

NYOTA wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz leo alifika ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM, yaliyopo Lumumba jijini Dar es Salaam na kukutana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Mpya wa CCM Shaka Hamdu Shaka. 

Katika ukurasa wake wa Instagram, mwekezaji huyo kijana aliandika: "Nimetumia wakati huo kumng'ata sikio juu ya matarajio yetu kwa Chama na Serikali katika Sekta ya Habari, Sanaa na Burudani, na amenihakikishia changamoto zote zitafanyiwa kazi na tabasamu litazidi kuonekana.

"Mwisho, Kama Kijana nimefarijika kuona Mwenyekiti wangu wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani anaendelea kuamini Vijana katika nafasi mbalimbali za Uongozi ndani ya Chama na Serikali, Katibu Mkuu wa CCM Kijana, Mwenezi Taifa wa CCM Kijana hili lina maana kubwa katika hili na mpongeza sana na ninawaomba Vijana na Watanzania wote wenzangu tumuunge Mkono, Mhe. Samia Suluhu Hassani ili mazuri aliyoyapanga katika Uongozi wake yaweze kutimia."

No comments