KAZI IMEANZA, JAMBAZI MMOJA AUAWA DAR


IGP Sirro amtoa Mambosasa Dar, amleta Wambura - Mwananchi

IKIWA ni siku moja tu baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala kuagiza Jeshi la Polisi kuwanyang'anya majambazi silaha kabla hawajazitumia, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kumuua Jambazi mmoja aitwae Kilambo Obale maarufu Nyasairo (44) mkazi wa Chanika.

Kamanda Camilius Wambura amesema Mtuhumiwa huyo alikamatwa May 27,2021 saa 5 usiku kwa makosa ya kujihusisha na ujambazi Mkoa wa Mara na Dar es salaam. 

Baada ya Mtuhumiwa kuhojiwa alikiri kujihusisha na matukio hayo na anamiliki silaha hivyo Askari walimwamuru kwenda kuonesha silaha hiyo ilipo na wakati walipofika eneo alipoifukia na kuanza kuchimba Mtuhumiwa alikurupuka na kukimbia kuingia kwenye maporomoko ya kingo za baharí.

Askari walipiga risasi hewani ili kumwonya asimame lakini hakutii na kuendelea kukimbia ambapo Askari walimpiga risasi ya mguu wa kulia kuanguka chini na baadae kufariki akipelekwa Hospitali ya Mwananyamala.

 

 

No comments