MBUNGE CATHERINE MAGIGE KUADHIBIWA NA CCM


MPEMBA WA PEMBA على تويتر: "Mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Arusha Mh Catherine  Magige ameitaka Serikali kujenga kwa kiwango cha Lami Barabara ya Kilomita  64 kuanzia King'ori Mpaka Ngarinanyuki Jimbo

KUFUATIA kitendo chake kisicho cha kimaadili cha kwenda kuleta vurugu katika msiba wa mtu anayemtaja kama mchumba wake, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimechukizwa na kulaani kitendo alichofanya Mbunge wake, Catherine Magige na kuahidi kumchukulia hatua.

Mbunge huyo jana Alhamisi Mei 27, 2021 alikwenda makaburini yalikokuwa yakifanyika mazishi ya mfanyabiashara Kuzula Madoda inayedaiwa kuwa ni mchumba wake. Madoda alifariki dunia Mei 24, 2021 na ameacha mke, Aziza Msuya na watoto.

Kitendo cha Catherine kwenda makaburini kiliibua hali ya sintofahamu kutokana na watu waliokuwa naye kuvunja geti na kuingia katika makaburi hayo ya familia.

Taarifa ya chama hicho iliyotolewa na katibu wa itikadi na uenezi, Shaka Hamdu Shaka leo Ijumaa Mei 28,2021 inaeleza kuwa CCM inaheshimu katika kujenga uimara wa familia, kuheshimiana ndani ya jamii na kuendeleza upendo katika familia halali badala ya mivutano na uvurugaji usiokuwa na sababu.

"Chama kinatafakari kwa undani kwa mujibu wa kanuni za maadili na katiba ya CCM na kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kimaadili kwa wote watakaothibitika kuwa sehemu ya matukio yaliyojenga kukiuka kwa katiba, kanuni na utamaduni wa kuheshimu na kuheshimiana uliojengeka ndani ya CCM," inaeleza taarifa hiyo.

No comments