KAMATI YASHAURI TANZANIA ITANGAZE CORONA IPO
KAMATI iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kutafiti kuhusu janga la Corona, leo imemkabidhi ripoti yao katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam huku ikiishauri serikali itangaze juu ya uwepo wa ugonjwa huo hapa nchini.
Licha ya kutaka itangaze uwepo
wake, pia imeshauri serikali iruhusu matumizi huru ya chanjo sahihi za Corona,
ikubali maazimio ya Kikanda na Kimataifa yanayotolewa juu ya Ugonjwa huo.
Kamati hiyo iliyoongozwa na Prof. Said Aboud ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, pia
imeshauri upanuzi wa maktaba za kupima, pia kuitaka serikali kutoa takwimu
sahihi za ugonjwa huo na kutaka tiba asili kuthaminiwa kisayansi.
Rais Samia Suluhu Hassan alipokea
ripoti hiyo leo'

Post a Comment