JICHO LA TATU BAO LA BERNARD MORISSON


MORRISON ATOKEA BENCHI NA KUFUNGA MABAO MAWILI SIMBA SC IKIICHAPA AL HILAL  4-1 DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE

 UKIONDOA mashabiki wachache wa watani wao wa jadi, Yanga, wengi wanakubaliana ndani ya mioyo yao kwamba Simba wako vizuri, ndani na nje ya uwanja. Why?

Ndani ya uwanja, wana wachezaji wenye viwango, wanaogombania namba. Wana kocha mzuri anayejua mbinu na ndiyo maana kutokuwepo kwa mchezaji yeyote, wa nafasi yoyote, haijawahi kuwa excuse kwa wao kushindwa. Ikitokea Simba imefungwa, kwamba flani hakuwepo, ni kauli ya wapinzani.

Nje ya Uwanja, they are well treated. Sisemi kuhusu malipo, lakini wanafika eneo la tukio kwa wakati, wanafikia hoteli ghali popote, iwe Tzee au nje na wana mashabiki wanaowapenda.

Njoo kuhusu bao la Morrison. Linatafsiri maana ya wachezaji wenye viwango. Kwanza unakubaliana na mimi, Morisson siyo chaguo la kwanza kikosini Simba, inabidi asubiri, asome mchezo then aingie ili alete tofauti.

Angalia lile bao lake la tatu kwa Simba dhidi ya Namungo; only a quality player can score. Mita tano tu kutoka katikati ya uwanja, anakunjuka na kupiga mpira wa vipimo, golikipa mzuri anahangaika hadi basi. Hakuna aliyemlaumu kipa, bali walimpongeza mpigaji.

Baada ya Azam Media kutupia hizo bilioni 225, ni matumaini yangu timu zetu zisajili wachezaji wenye viwango, ambao hata hapa Bongo wapo, ili ligi yetu isiwe ya upande mmoja. Just imagine, timu zimecheza mechi 30, lakini inayoongoza imecheza mechi 26 tu, tena ikiwa na idadi kubwa ya mabao ya kufunga na ikifungwa machache kuliko zote.

Weka ushabiki pembeni, ligi yetu haina uwiano baina ya Simba na timu zingine.

 

 

No comments