JEURI YA FEDHA KATIKA LEVO ZINGINE JAY Z NA BEYONCE


Beyonce and Jay Z Marriage, Relationship, Kids

WANANDOA Jay-Z na Beyoncé ambao ni moja ya couple zinazochukuliwa kama mfano kwa mastaa wa Marekani, wameandika historia kwa mara nyingine tena kwa kuagiza kutengenezewa gari ghali zaidi ulimwenguni.

Mtandao wa PageSix unaripoti kuwa Jay Na Bey wamelipa US dola milioni 28, sawa na shilingi za kitanzania bilioni 64, kununua gari la kifahari aina ya Rolls Royce BoatTail Convertible lililotengenezwa kutokana na matakwa yao.

Roll Royce ya Blue na imepambwa na vitu vyote wanavyopenda Couple hii.

Jay Z na Beyonce hupenda kushirikiana kununua vitu pamoja tofauti na wanandoa wengi maarufu duniani, tambua kwa sasa wanaishi kwenye nyumba walionunua pamoja yenye thamani ya US Dola milioni 88 (Wanailipia kwa muda wa miaka 30) kwenye mitaa wanayoishi mastaa na matajiri huko Bel-Air, Los Angeles, California.

Jumba hilo lina vyumba 8 vya kulala, mabafu 11, eneo la kuegesha magari 15, mabwawa ya kuogelea manne na uwanja wa mpira wa kikapu. 

No comments