JAKAYA NI MZIMA WA AFYA - RIDHIWANI
KUMEKUWA na taarifa katika baadhi ya mitandao ya kijamii, ikisema kuwa Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete ni mgonjwa. Habari hizo zinasambaa kwa kasi.
Hali hiyo imesababisha watu wa
karibu na familia hiyo kupiga simu na kutuma ujumbe kwa wanafamilia wakitaka
kujua ukweli.
Mtoto wa kiume wa Jakaya, ambaye pia
ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete amekanusha taarifa za sintofahamu
zilizosambaa kupitia mitandao ya kijamii zikimhusishia baba yake mzazi na rais
mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete.
Kupitia akaunti yake ya Twitter,
Ridhiwan ameandika:
"Baada ya kupokea Simu na Jumbe mbalimbali nimeona
nitumie nafasi hii kuweka kumbukizi sawa. Mzee wetu na Mzazi wetu Dr. Jakaya
Mrisho Kikwete yupo salama wa afya nyingi sana. Hana tatizo lolote kiafya na
anaendelea na majukumu yake. Taarifa za aina yeyote ni za Kipuuzi na za
kupuuzwa"...

Post a Comment