INAWEZEKANAJE DAWA ZIPULIZWE VYUMBA VYA WACHEZAJI?


My Dar es Salaam on Twitter: "Reflect on the #legacy ❤️ The National Stadium,  Also known as Benjamin Mkapa Stadium. A 60,000 seats multipurpose stadium  initiated by former president Benjamin Mkapa who

 KELELE za timu mbalimbali juu ya tabia ya timu moja kupuliza dawa katika vyumba vya wachezaji wapinzani zinazidi kuwa nyingi na ya hivi karibuni ni ya jana kutoka kwa viongozi wa klabu ya Dodoma Jiji wakiilalamikia Simba.

Katika mchezo huo wa jana, wageni hao kutoka Dodoma walisalimu amri baada ya kupigwa mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Hizi ni kelele za siku nyingi na mtuhumiwa namba moja mara nyingi amekuwa ni Simba. Hebu tujiulize, jambo hili linawezekanaje na wahusika wote wabaki kimya?

Viongozi wa Uwanja

Huu ni uwanja wa serikali na una uongozi wake kamili kwa maana ya meneja na wafanyakazi waajiriwa. Kuna mtu mwenye jukumu la kuangalia sehemu ya kuchezea (pitch), kuna mtu wa kusimamia usafi wa majukwaa, vyumba na mwisho kabisa walinzi. Hivi hawa wote wapo wapi hadi jambo hili linafanyika kila siku?

Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo

Hawa ndiyo wasimamizi wa huu uwanja kwa niaba ya serikali. Ni jukumu lao kwa hiyo kuhakikisha tuhuma kama hizi zinakomeshwa ama kwa kuanika ukweli au kukanusha.

Wizara inao madaktari wa binadamu na inao wataalamu wa afya wenye uwezo wa kutambua madawa ya aina mbalimbali. Wanaweza kujua chumba hiki, siku fulani kilipuliziwa dawa aina hii, yenye madhara haya na yale. Mbona hawaifanyi hii kazi?

TFF mbona wananyamaza wakati soka likichafuliwa?

Unashangaa kwa nini Shirikisho la Soka nchini TFF linakaa kimya wakati mchezo wa soka unachafuliwa. Kitendo cha timu kulalamikiwa kwa kupulizia dawa timu pinzani ili icheze chini ya kiwango waweze kushinda, ni hujuma kwa TFF inayotaka soka la haki na ushindani ndani ya uwanja.

TFF ina wataalamu wa kujitegemea wenye uwezo wa kuondoa utata huu. Kama ni kweli Simba wana tabia hiyo, ikithibitishwa, wachukuliwe hatua stahiki ili mradi mchezo huu ubakie kuwa wa kuzingatia sheria 17.

Kama lenyewe linashindwa, linaweza kuomba msaada kutoka Caf au hata Fifa ili mradi malalamiko haya ambayo lengo lake ni kuipaka matope image ya soka la Tanzania yaondolewe kabisa.

Simba wenyewe wanasemaje?

Ni jambo la ajabu kidogo kuona wanaotuhumiwa mara nyingi, ambao ni Simba wamekaa kimya. Inawezekana ni kweli wameamua kupuuza kwa sababu hawahusiki, lakini uongo unaposemwa sana na wenye wajibu wa kukanusha wakakaa kimya, huonekana ni ukweli.

Maana isije ikawa kuna watu wanacheza na saikolojia ya timu pinzani. Watu wanaweza kuja kupuliza manukato chumbani, lakini kwa hofu iliyojengwa, hujikuta wakiamini ni dawa za kupunguza uwezo.

All in All, wahusika lazima wasimame na kusema ukweli.

No comments