CHADEMA YAKATAA KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025

 

Chadema chairman Freeman Mbowe to be a free man today - The Citizen

CHAMA Kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema hakitashiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 hadi pale Katiba Mpya itakapopatikana na kuwepo kwa Tume Huru ndani yake.

Msimamo huo umetolewa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe wakati akizungumza katika kikao chake na viongozi wengine wa Kanda ya Kaskazini jijini Arusha.

Jambo hilo limezua maoni mengi tofauti kutoka kwa wadau na hivyo kusababisha hali hiyo kuzua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii hivi sasa.

No comments