IJUE SIMULIZI YA MEDIA TYCOON VLADIMIR GUSINSKY NA PUTIN

MNAMO mwaka wa 1999, kulikuwa na
muungano/umoja wa kisiasa ambao uliwajumuisha rais wa wakati huo wa Urusi, Borris
Yeltsin, jamaa zake na Yeltsin, pamoja na kundi la wafanyabiashara mwenye nguvu,
wanaojulikana kama Family, ambao ndio inasemekana walimleta Vladimir Putin kama
mrithi pekee wa Rais Yeltsin.
Wakati huo huo, Vladimir Gusinsky alijiweka
nje ya kikundi hicho chenye nguvu cha Family na kwa sababu hiyo alituhumiwa
kuunga mkono makundi ya upinzani yaliyokuwa yakienenda kinyume na matakwa ya
Kremlin (Ikulu ya Russia). Na huu ndio ulikuwa mwanzo wa mzozo kati ya
pedeshee/papaa Gusinsky, kikundi cha watoto wa mjini cha Family, pamoja na
Luteni Kanali Vladmir Putin.
Mnamo Septemba mwaka 1999 kulikuwa na
mashambulio kadhaa ya kigaidi huko jijini Moscow na miji mingine nchini Urusi.
Majengo kadhaa yalilipuliwa kwa mabomu na watu wengi sana waliuawa.
Kremlin/Ikulu ya Urusi ilichukua msimamo wa kuamini kwamba makundi ya magaidi
wa Chechen ndio waliokuwa wanahusika na mabomu hayo.
Wakati huo huo, kikundi cha majirani waliokuwa
wanaishi katika jengo la ghorofa kumi pale jijini Moscow walikutana na idadi
kubwa ya vilipuzi/explosives chini ya jengo lao, na wakaripoti kwa Police/FSB.
Wakati huo kundi la wachunguzi wa waandishi wa habari wa kujitegemea walifunua
funua ukweli fulani ambao uliunganisha vilipuzi vile na watu walio na uhusiano
na Police/FSB.
Television ya NTV ya bwana Gusinsky kwa
kupenda sifa ya kufurahisha mabeberu iliamua kuchukua msimamo na kufanya
uchunguzi wa kina kama waandishi wa habari - ikichunguza uwezekano wa kwamba
Police/FSB ilikuwa ikitengeneza milipuko kwa makusudi katika juhudi za
kushawishi uchaguzi ujao na kuhakikisha kundi la Family linashinda.
Ukweli kwamba kituo cha NTV cha bwana Gusinsky
kilianza uchunguzi juu ya milipuko ile
kilisababisha hasira kali sana huko Ikulu/Kremlin; kwa kweli, Gusinsky alipewa
tamko kali la kuondoa uchunguzi ule wa huru kutoka katika kituo chake cha NTV,
laa sivyo atakabiliwa na athari ambazo hakuzitarajia.
Gusinsky alikataa katakata kusitisha uchunguzi
ule. Kwa kuongezea tu ni kwamba, wadau mbalimbali wa kujitegemea (bila shaka ni
vibaraka wa mabeberu) waliishutumu ikulu ya Kremlin na Kanali Putin kwa kuandaa
milipuko ile, na kusababisha vita mpya vya Chechen, kwa lengo la kujiongezea
umaarufu katika mchakato wa uchaguzi uliokuwa unafuata.
Hii ilikuwa hatua ya mwisho ya kuvunjika kwa
uhusiano mwema uliokuwapo mwanzo baina ya Gusinsky na Kremlin, kikundi cha
watoto wa mjini cha Family, pamoja na mrithi wa Yeltsin ambaye ni Putin. Mnamo 31
Disemba 1999 Rais Yeltsin alijiuzulu, na Vladimir Putin alikua rais mteule wa
Urusi. Putin alikaimu kiti kwa muda kabla ya kula kiapo.
Kujiuzulu kwa Yeltsin kulimleta Putin kuwa
Kaimu Urais wa muda wa Russia, na uchaguzi uliofuata mnamo mwezi Mei mwaka 2000
ulimleta Putin mamlakani bila pingamizi.
Moja kati ya matendo ya kwanza kukosolewa
hadharani ya rais mpya Putin ilikuwa kuanza kwa uchunguzi dhidi ya Gusinsky kwa
lengo la kuiweka NTV chini ya udhibiti wa serikali na kuwanyamazisha wapinzani.
Mnamo mwezi wa Juni, ofisi ya Mwendesha
Mashtaka Mkuu wa serikali ilizindua uchunguzi dhidi ya Gusinsky kwa matumizi
mabaya ya pesa (Money Laundering) yakihusiana na kampuni ya utengenezaji ya
video ya nchini Urusi iliyokuwa inamilikiwa na ndugu wa bwana Gusinsky. Mnamo
mwezi Juni tarehe 13 alikamatwa huko jijini Moscow na kuwekwa lupango/ndani.
Muda mfupi baada ya kukamatwa, wawakilishi wa
Gusinsky walipendekeza kwa Ikulu ya Kremlin kuuza vyombo vile vya habari kwa
kampuni ya serikali ya Gazprom-Media kwa bei ambayo Gazprom-Media inataka, ya
Dola za Kimarekani milioni 300, ili pedeshee/papaa Gusinsky aweze kupata uhuru
wake.
Baada ya siku tatu za shinikizo kubwa la umma,
Gusinsky aliachiliwa kutoka gerezani na kuwekwa kizuizini nyumbani kwake mnamo
mwezi wa Juni tarehe 16. Wiki kadhaa baadaye, mnamo mwezi wa Julai, alisaini
makubaliano ya kuuza vyombo vyake vyote vya habari kwa Dola za Kimarekani
milioni 300.
Mchakato wa mauzo ulisainiwa na naibu Waziri
wa wakati huo katika nafasi yake kama mkuu wa Wizara ya Habari, Utangazaji na
Mawasiliano ya Shirikisho la Urusi.
Uchunguzi/upelelezi wa makosa ya jinai dhidi
yake ulifungwa, na Gusinsky aliondoka Urusi mara moja. Kuanzia wakati huo
Gusinsky hakuwahi kurudi teeeeeeeeeenaaa Urusi.

Post a Comment