IGP SIRO: KINONDONI KINARA WA UHALIFU TANZANIA

WAKATI wimbi jipya la ujambazi was kutumia silaha, mauaji, uporaji na vibaka wakirejea kwa kasi katika maeneo mbalimbali nchini, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, ameutaja mkoa wa Kipolisi wa kinondoni kama kinara wa uhalifu nchini.
IGP Sirro amesema hayo jijini Dar es salaam,
wakati akizungumza na Wenyekiti wa Serikali za Mitaa, watendaji Kata, pamoja na
watendaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi ambapo amewataka watendaji wote
kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha usalama unaendelea kuimarishwa.
Aidha, IGP Sirro ametoa muda wa wiki moja
kuhakikisha wanakomesha vitendo vya kihalifu kwa kushirikiana na watendaji
wengine huku akitoa wito kwa mgambo kuacha kujiingiza kwenye vitendo vya
rushwa.
“Tutaendelea kutekeleza wajibu wetu kwa
kuzingatia uzalendo, taratibu na kanuni na kuhakikisha maeneo yetu na wananchi
tunaowahudumia yanakuwa salama”,amejibu Mohamed Mawal, Mwenyekiti wa Serikali
ya Mtaa wa Tegeta huku Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mlalakuwa Suleiman
Masare, akiahidi kutoa pikipiki mpya kwa Kituo cha Polisi Chuo Kikuu
itakayosaidia kurahisisha utoaji wa huduma za kipolisi kwa wananchi.
Kabla ya kukutana na watendaji wa serikali za
mitaa na watendaji wa kata na watendaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi pia
IGP Sirro, alifanya kikao kazi na maofisa na askari wa Jeshi hilo ambapo
aliwataka kuendelea kutimiza wajibu wao na kuwachukulia hatua kali
wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu.

Post a Comment