GARI LA AKON LAIBWA KITUO CHA KUJAZIA MAFUTA

TAARIFA iliyotolewa hivi punde na tovuti ya habari za burudani #TheShadeRoom imeripoti kuwa gari ya staa wa muziki kutokea nchini Senegal, Akon imeibiwa.
Kwa mujibu wa #Fox5Atlanta gari hilo
limeibiwa wakati ambapo nyota huyo akiwa katika kituo cha kujaza Mafuta huko
Sydney Atlanta, ambapo mtuhumiwa alirukia ndani ya mchuma huo akaliwasha na
kukimbia nalo.
Taarifa zinaeleza gari hilo aina ya SUV ndilo lililokuwa
likimilikiwa na staa huyo na kuibiwa.
Hata hivyo, idara ya polisi ya Atlanta wapo katika uchunguzi
ili kumbaini mtuhumiwa aliyehusika na kitendo hicho cha kihalifu.

Post a Comment