HAKUNA MISHAHARA MIPYA

RAIS Samia Suluhu
Hassan leo amehutubia katika kilele cha siku ya wafanyakazi duniani, lakini
tofauti na matarajio ya wengi, amekataa kupandisha mishahara.
Amesema ni mapema
mno kwake kuweza kupandisha mishahara wiki chache tu tangu achukue madaraka,
lakini akatoa ahadi kuwa atafanya hivyo siku zijazo.
Hata hivyo, pamoja
na mishahara kutokupanda, kodi ya mshahara inapunguzwa, Tozo ya asilimia 6
kwenye makato ya Bodi ya Mikopo imefutwa, watumishi wanapandishwa madaraja, na
ukomo wa umri wa wategemezi kwenye Bima ya Afya umeongezwa kutoka miaka 18 hadi
21.
Wachumi wsengi
hawakutegemea mishahara kupanda kwani kampuni na mashirika mengi, ya umma na
binafsi yameyumba kutokana na athari za Covid-19.

Post a Comment