GARI LA BAJETI YA BARABARA WILAYANI BONGO LAUNDWA


Bugatti's 'La Voiture Noire' Is the Most Expensive New Car Ever Sold

KAMPUNI ya kutengeneza magari ya thamani zaidi duniani ya Bugatti, imetengeneza gari la bei mbaya zaidi duniani kwa sasa, likiwa na thamani ya shilingi za kitanzania, bilioni 41.7 zinazoweza kutengeneza barabara kwa kiwango cha lami katika wilaya moja nchini Tanzania.


Katika hali isiyo ya kawaida, kampuni maarufu ya kutengeneza magari ya kifahari zaidi duniani ya 
@bugatti imekamilisha gari yake ya "La Voiture Noire" lenye thamani zaidi duniani litakalouzwa Dola za Marekani milioni 18 sawa na Sh bilioni 41.7 za Kitanzania. 

Wataalamu wa magari ya kifahari wanasema gari hilo ndio la gharama kubwa zaidi kuwahi kutengenezwa duniani.

Inaripotiwa kwamba gari hili jipya limewaacha midomo wazi watu wengi duniani ikiwamo matajiri wenye ‘pepo la magari ya kifahari’ 

#Bugatti ni miongoni mwa kampuni kubwa inayosifika kwa kutengeneza gari imara na bora zaidi duniani na kufanya kuwavutia watu wengi wenye uwezo mkubwa kumiliki gari hizi licha ya bei zake kuwa za gharama za juu sana


No comments