ECOWAS NAYO YATISHIA KUIWEKEA MALI VIKWAZO VIPYA

SIKU chache tu baada ya Marekani na Jumuia ya Ulaya kuonya
juu ya kuiwekea vikwazo nchi ya Mali baada ya Jeshi kufanya mapinduzi, Jumuiya
ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) nayo imeonya kuwa inaweza
kurejesha vikwazo nchini humo kufuatia Kanali Assimi Goita kuchukua
madaraka.
Kanali Goita ameitwa kwenye Mkutano wa Dharura wa Viongozi wa
Afrika Magharibi Nchini Ghana ambapo mapinduzi ya pili ya Mali
katika miezi 9 yatajadiliwa.
ECOWAS inahofia mabadiliko hayo yanaweza kuyumbisha utulivu
na kudhoofisha mapigano ya Kikanda dhidi ya vikundi vinavyohusiana na Al-Qaeda
na ISIS.

Post a Comment