DUH, MAPATO YA TIMU ZENJI KATIKA LIGI HAIKUBALIKI

HUKU Shirikisho la Soka la Zanzibar ZFF likiendelea na jitihada zake za kutaka
kutambuliwa kama chama huru katika Cecafa, Caf na Fifa, mapato ya timu
zinazoshiriki Ligi Kuu Zanzibar ni ya kukatisha tamaa.
Kwa mujibu wa viongozi wa klabu mbili za huko,
zimekiri kupokea shilingi 3,000 kila mmoja, ikiwa ni sehemu ya mapato baada ya
makato ya gharama zingine za uwanja uliopigwa Mao Ze Dong.
"Mbona hii kawaida kwetu hasa mechi tunazocheza uwanja
wa Mao, siku nyingine tunapata 1,000, 500 au hatupati kabisa, kwa hiyo hii elfu
3 kwetu wala hatujashangaa”- alisema kiongozi wa timu ya Malindi, Masoud.
"Ni kweli na sisi Kipanga tumepata elfu tatu tu, lakini
mbona hii kawaida tumeshazoea"-alisema Kiongozi mmoja wa Kipanga ambaye
hakutaka jna kake litajwe.

Post a Comment