CRISTIANO RONALDO ATAMBAA NJIA YA JACKO WACKO


Cristiano Ronaldo wants his son to become the 'best in football or  medicine', and he's 10

UNAMKUMBUKA Legendary wa muziki wa Pop duniani, Michael Jackson wa Marekani? Jamaa alikuwa anawazingua sana wamarekani weusi, hasa alipokuwa anafanya juhudi kubwa kuukana weusi wake, akitaka kujifananisha na wazungu.

Hata hivyo, uwezo wake na ubunifu wake kazini, ulimfanya apate heshima kutoka jamii za watu wote wa taifa hilo kubwa zaidi duniani. Na kuna jambo moja alilolifanya, likamfanya awe wa kipekee.

Jamaa hakuwahi kuoa ingawa alifariki akiwaacha wanae watatu. Hawa wote aliwapata kwa makubaliano na mama zao, akipandikiza mbegu. Hii maana yake ni kuwa vijana wale wa Jacko Wacko, hawamjui mama yao.

Hivi ndivyo ilivyo kwa mwanasoka nyota duniani, Cristiano Ronaldo.

Mtoto wa kwanza wa Ronaldo, Cristiano jr, ni mtoto aliyetokana na makubaliano ya kimkataba kati ya nyota huyo na mwanamke mmoja nchini Marekani, ambako kazi yake ni kuzaa tu, baada ya hapo analipwa chake maisha yanaendelea.

Mkataba ulisema baada ya kuzaa, atalipwa pesa na hivyo kupoteza haki zote za mtoto na haruhusiwi kujitangaza, vinginevyo atalazimika kulipa malipo makubwa.

Kitendo hiki kinaitwa Surrogacy, mama anayezaa mtoto anaitwa Surrogate Mother, ni makubalino ya kisheria, ukasainiwa kati ya Ronaldo na mwanamke mbele ya Wanasheria wa pande zote mbili.

Hii pia hakuishia kwa Cristiano Jr tu bali hata watoto wake mapacha Mateo na Eva nao walizaliwa kwa mkataba kati ya Mama wa watoto na Ronaldo.

No comments