CCM WABABE UCHAGUZI MDOGO MUHAMBWE

 


Dailynews


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka mbabe katika Uchaguzi mdogo Jimbo la Muhambwe baada ya Msimamizi wa Uchaguzi , Diocles Rutema kumtangaza mgombea wa chama hicho, Dkt Florence George Samizi kuwa mshindi.

Msimamizi huyo wa uchaguzi alitangaza kuwa mshindi alipata idadi ya kura 23,441 sawa na asilimia 67% ya kura zote akifuatiwa na Mgombea wa Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), Masabo Julius aliyepata kura 10,847 na Mgombea wa Democratic Party (DP), Philipo Fumbo akipata kura 368.

No comments