CCM PIA WAIBUKA WASHINDI JIMBO LA BUHIGWE

FELIX Kavejuru ambaye aligombea Ubunge kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), katika jimbo la Buhigwe, ametangazwa kuwa mshindi wake baada
ya kuwabwaga wapinzani wake 12 wengine.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la
Buhigwe, Marycelina Mbehoma alimtangaza Felix Kavejuru katika uchaguzi
uliofanyika Mei 16, 2021, kwamba alipata kura 25,274 kati ya kura 30320 halali
zilizopigwa. Hivyo Ndugu Felix Kavejuru ndiye Mbunge mteule jimbo la Buhigwe
kwa tiketi ya CCM.
Uchaguzi huo ulifanyika ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi
baada ya alikyekuwa mbunge wake, Philip Isdor Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufuatia kifo cha Rais John Joseph
Magufuli.

Post a Comment