BOSI WA YANGA KUMJENGEA NYUMBA MWAKINYO

MFANYABIASHARA maarufu nchini ambaye pia aliwahi kuwa kiongozi wa Klabu ya Yanga, ambao ni mabingwa wa kihistoria katika Ligi Kuu Bara, Davis Mosha ameahidi kum-support Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo kwenye mambo mbalimbali ikiwemo kwenye ujenzi wa nyumba yake.
“Ni kijana anapenda fani yake nimeona nim-support kwenye
mambo mengi kwa mfano akija Dar es salaam huwa mimi ndio nam-take care kila
kitu na nina zawadi niliahidi nitampa sababu ametufurahisha Watanzania”
“Kuna mambo mengi nimemuahidi kum-support, nimemwambia sasa
hivi atafute kiwanja ili tuweze kum-support aweze kujenga nyumba yake na mimi
ni miongoni mwa Watu wanaotaka kum-support ajenge nyumba yake”
Juzi, Mwakinyo alimtwanga bondia
kutoka Angola na kufanikiwa kutwaa mkanda wa Afrika.

Post a Comment