BOSI GSM AIPONGEZA AZAM MEDIA
KUFUATIA kitendo cha Kampuni ya Azam Media Ltd cha kutiliana saini mkataba wenye thamani ya shilingi bilioni 225.6 na Shirikisho la Soka Nchini TFF kama haki za matangazo ya televisheni kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, bosi wa makampuni ya GSM amepongeza hatua hiyo.
Ghalib Said
Mohammed, ambaye kampuni yake inaidhamini Yanga ambao ni mabingwa wa
kihistoria, amesema kitendo hicho kinastahili pongezi kwani kinatoa chache kwa
vijana wa kitanzania kujituma ili kutumia fursa hiyo kikamilifu.

Post a Comment