BASATA KUANZA KUWABANA WASANII LEO



LEO Mei 1 2021 ndio siku rasmi ambayo Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) linaanza kutumia kanuni ya kuzipitia nyimbo mpya za Wasanii wote Tanzania kabla ya kupelekwa kwenye Radio na televisheni.

 “hii sio sheria mpya, ilikuwepo kabla ila haikua imeanza kutekelezwa"

Naibu Katibu Mtendaji wa BASATA Matiko S. Mniko amenukuliwa akisema;

"Kuanzia tarehe 1 tutaanza kufanya oparesheni ya wale ambao hawafati utaratibu huu, kwa sababu ya umuhimu wa utekelezaji wa kanuni hii, tuliunda kamati ambayo imejipanga kwa ajili ya kuhakikisha kwamba kazi zote zinahakikiwa na hakuna ambae atacheleweshewa"

"Kanuni hii inataka Msanii kupeleka wimbo wake wa audio au video kwenye Baraza hilo kwa ajili ya kupitiwa/kukaguliwa kwanza kabla ya kuuachia kwenye chombo chochote cha habari, ukishakaguliwa na kupitishwa, BASATA itatoa cheti maalum cha uthibitisho ambacho Msanii atatakiwa kwenda nancho kwenye Radio/TV na kukionesha ili wimbo wake uanze kuchezwa."

No comments