TETESI: DIAMOND AMENUNUA PRIVATE JET?


1999 CHALLENGER 604 (11028296)


Kuna tetesi zinasambaa mitandaoni kuwa msanii mkubwa Tanzania, Diamond Platnum amenunua ndege binafsi.

Vipande vya video vinavyotoka kwa mmoja wa mameneja wake, Sallam zinaonyesha picha za mwekezaji huyo kijana akiingia katika 'show room' ya ndege ndogo, ishara kwamba amekwenda kwa ajili ya malipo.

Aidha, katika akaunti yake kwenye mtandao wa Instagram, msanii huyo ameweka maneno ya kushukuru, akisema Alhamdulilah, jambo linalotafsiriwa kuwa huenda ni kwa kutimiza ndoto zake za muda mrefu.

Miaka kadhaa iliyopita, mwimbaji huyo kutoka Tandale aliwahi kudokeza kuwa ana lango la kununua ndege binafsi ili kurahisisha shughuli zake za kisanii na kibiashara. 

No comments