JAJI KIONGOZI: WANAOPELEKA KESI BILA USHAHIDI WACHUKULIWE HATUA

Jaji Kiongozi wa Mahakama ya
Tanzania Dkt. Eliezer Fereshi ameagiza ngazi mbalimbali za mamlaka zinazohusika
kufanya usuluhishi kuchukua hatua kwa watu au taasisi zinazopeleka kesi
Mahakamani bila ya kuwa na ushahidi na kupelekea kuwepo kwa mahabusu wengi gerezani
na kesi kuchukua muda mrefu.
Ameyasema hayo wakati akizindua jengo la mahakama ya wilaya
ya Kasulu Mkoani Kigoma na kuongeza kuwa Mahakama inaendelea kuhakikisha wilaya
zote nchini zinakuwa na majengo yake, kuongeza watumishi na vitendea kazi sambamba
na kutumia teknolojia kurahisisha usikilizwaji wa mashauri.

Post a Comment