CHAMA MCHEZAJI BORA WA WIKI CAFCL
KIUNGO mtengeneza
mipango wa Simba, Clatous Chota Chama 'Triple C' au maarufu kama Mwamba wa
Lusaka, ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa raundi ya tano ya michuano ya Klabu
Bingwa Barani Afrika.
Katika mchezo wa
raundi ya tano uliochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam
April 3 mwaka huu, kati ya Simba na AS Vita, Chama alifunga mabao mawili na
kutoa assist moja na hivyo kuhusika katika mabao matatu.
Hii ni mara ya pili
kwa klabu ya Simba kutoa mchezaji bora wa wiki katika michuano hiyo. Mara ya
kwanza ilikuwa ni katika mchezo wa raundi ya pili katika ya Simba na Al Ahly
jijini Dar es Salaam, ambapo mchezaji Luis Minniqsonne alifunga bao pekee la
ushindi kwa Simba na bao lake likiwa ni bora wiki hiyo.

Post a Comment