SENEGAL, TISHIO LA TANZANIA TIMU NNE MSIMU UJAO

 Inaweza kuwa picha ya maandishi yanayosema 'CAF TOTAL CHAMPIONS LEAGUE CAF TOTAL CONFEDERATION CUP'


 

SIYO habari rafiki sana kwa familia ya soka nchini Tanzania, kwani hadi jana, bado hakuna uhakika wa asilimia mia moja kuingiza timu nne katika kampeni za michuano ya kimataifa ya Afrika.

Hii ni baada ya jana, Al Ahli Benghazi ya Libya ikiwa ugenini kwenye mchezo wa mwisho wa kombe la shirikisho (Caf Confederation Cup) kufungwa 1-0 na Es Setif ya Algeria na kushindwa kufuzu robo fainali.  Baada ya Benghazi kushindwa kufuzu, nchi ya Libya imebaki na pointi 13.5 ambazo haziwezi kuongezeka.

Tanzania baada ya timu ya Simba kufuzu robo fainali ya Caf Champions League na Namungo kumaliza nafasi ya nne kwenye makundi ya Caf Confederation Cup, sasa tuna pointi 27.5 ambazo zinaweza kuongezeka ikiwa Simba itafanikiwa kufuzu nusu fainali ya Klabu bingwa Afrika.

Baada ya Libya kushindwa, mshindani wetu kwa sasa ni Senegal ambayo haikuwa na pointi zaidi ya timu zao 2 kufanya vizuri msimu huu ambazo ni timu ya Teungueth FC iliyoshiriki klabu bingwa Afrika na kuishia nafasi ya nne kwenye makundi huku ASC Jaraaf imefanikiwa kufuzu robo fainali ya kombe la shirikisho kama nchi Senegal wana Pointi 15 sasa.

-Nchi ya Senegal pointi zake zinaweza kuongezeka kwa sababu ya Klabu ya ASC Jaraaf kufuzu robo fainali ya kombe la shirikisho (Caf Confederation Cup) ila mpaka atuzidi sisi Tanzania mpaka timu yao ya ASC Jaraaf iwe bingwa wa Kombe la Shirikisho (atakuwa amefikisha pointi 30) huku aiombee timu ya Simba itolewe robo fainali ili sisi (Tanzania) tubaki na Pointi 27.5 

No comments