LEICESTER WAHOFIA KUTUPWA TENA NJE CL

KLABU ya soka ya Leicester
ambayo hadi sasa inashika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu ya England, inahofia
huenda ikatupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwa mara pili
mfululizo, HATA KAMA itamaliza ikiwa ndani ya Top Four.
Hata hivyo, hiyo
itatokea tu iwapo Chelsea na Arsenal zitashinda makombe ya Ulaya, ambako timu
hizo mbili zimefikia hatua ya fainali.
Chelsea inashiriki
Ligi ya Mabingwa wakati washika mitutu wa London, wapo Europa League.
Kikosi hicho cha
kocha Brendan Rodgers kipo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi
62, nne nyuma ya Chelsea. Ili kucheza michuano ya Ulaya mwakani, italazimika
kupigana kuhakikisha inamaliza ligi ikiwa nafasi hiyo hiyo.
Lakini wakishika
nafasi ya nne, na majirani hao wa London wakashinda mataji, watajikuta nje ya
michuano ya Ulaya kwa vile Shirikisho la soka barani Ulaya, hutoa nafasi hadi
tano tu kwa timu za nchi moja kushiriki michuano yake.
Msimu uliopita, Leicester
nusura icheze Ligi hiyo ya Mabingwa baada ya kufanya vyema kabla ya kuporomoka
kiwango kufuatia lockdown ya Covid 19 na kujikuta wakipokea kipigo toka kwa Man
United katika mechi yao ya mwisho iliyowafanya wacheze Europa League.

Post a Comment