NYALANDU, METHEW WAREJEA CCM

 


ALIYEWAHI kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika serikali ya Awamu ya nne, Lazaro Nyalandu ambaye alikihama chama hicho Septemba mwaka 2017 na kujiunga na chama kikuu cha Upinzani nchini, Chadema, amerejea katika chama tawala.

Nyalandu ambaye alikuwa ni Mwenyekiti  wa Kanda ya Kati wa Chadema  na Mjumbe wa Kamati Kuu, amejiunga na chama hicho leo, wakati wa mkutano mkuu maalum uliokuwa na lengo la kumkabidhi Rais Samia Suluhu Hassan Uenyekiti wa chama hicho kikongwe.

Wakati wa hotuba yake mbele ya mkutano huo, Nyalandu, pamoja na mambo mengine, aliwaomba radhi wanachama wa CCM kwa kitendo chake hicho cha kuhama chama.

Wakati huo huo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kusini, Seleman Methew naye amejiunga na chama hicho tawala, akidai ndicho kilichomkuza kisiasa.

 

No comments